Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 2 May 2015

KUPUMZIKA NI MUHIMU KWA AFYA YAKO, TUMIA WEEKEND YAKO VIZURI
Je, huwa unapata nafasi ya kunapumzika? Kama ndiyo huwa unadhani ni muhimu kufanya hivyo?


Kupumzika angalau kidogo kila siku, husaidia sana kuongeza umakini zaidi bila kuchoka katika shughuli zako za kila siku.

Kutokana na umuhimu wa kupumzika ni vyema ukaanza kutenga muda wa kupumzika na utambue kuwa muda wa kupumzika hauji wenyewe ila ni wewe mwenyewe ndio unaowajibu wa kutafuta wakati wa kupumzika walau kidogo kila siku.

Tunapozungumzia kupumzika ni pamoja na kupata usingizi wa kutosha. Wataalam husema binadamu anahitaji muda usiopungua saa nane za kulala kila siku. 

Hivyo kama unaipenda afya yako ni vyema kuanzia weekend hii ukaanza kuhakikisha unatenga muda wako wa kupumzika pamoja na kufanya mazoezi japo kidogo kila siku.

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.
 

No comments:

Post a Comment