Friday, 8 May 2015

LEO NAKUPAA HII FAIDA YA KUTUMIA MBEGU YA PARACHICHI KATIKA TIBA
Habari za Ijumaa ya leo msomaji wetu wa www.dkmandai.com napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha katika muendelezo wetu wa kufahamishana namna mimea na matunda yanavyoweza kuwa msaada mzuri katika afya zetu.
Leo tena nimekuja na hii faida nyingine ya parachicihi, lakini leo tiba itahusika zaidi katika matumizi ya mbegu ya parachichi yenyewe yaani ile inayokuwa katikati ya tunda la parachichi.

Mbegu ya parachichi inaweza kuwa tiba kwa wale wenye shida ya kupata maumivu na kukwama kwa haja ndogo (mkojo).

Ili mbegu hii ya parachichi iweze kuwa tiba ya tatizo hilo ni lazima kwanza isagwe hadi iwe unga kabisa na kisha kukaangwa kidogo. Baada ya zoezi hilo kukamilika mhusika (mgonjwa) atakuwa akitumia vijiko viwili vya unga huo kwa kuchanganya na maji ya moto kikombe kimoja na kunywa.

Mgonjwa atatakiwa kutumia tiba hii kwa muda wa wiki kadhaa hadi pale atakapoona mabadiliko katika tatizo hilo.

Asante sana kwa kuendelea kuwa karibu nasi, kama unatatizo lolote la kiafya unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na pia unahaki ya kuwasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Kisha utatuambia tatizo lako nasi tutakuwa tayari kuweza kukusaidia.

No comments:

Post a Comment