Saturday, 30 May 2015

LEO NI CHOROKO KATIKA TIBA


Habari za wakati huu mdau na mfuatiliaji wetu wa www.dkmandai.com karibu tena tuangalie faida za baadhi ya vyakula vyetu.

Kwa sasa wacha tuangalie hizi faida za kutumia choroko kiafya.

Kama wewe ni miongoni mwa wale watu wengi ambao hutumia choroko katika mlo wao, basi utakuwa ni miongoni mwa watu wanopata faida za virutubisho hivi vifuatavyo:

Choroko ni kati ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha protini na madini ya phosphorus, calcium , lakini pia choroko husaidia sana kuimarisha mifupa mwilini.

Mbali na hayo, choroko pia husaidia sana kwa afya ya moyo kutokana na mafuta yalipo ndani yake kuwa ni salama, lakini pia husaidia sana katika masuala ya umeng’enywaji wa chakula tumboni.

Pamoja na hyo choroko ina vitamin B1, B2 ambayo husaidia sana kuimarisha mfumo wa fahamu

Unaweza kuwasiliana nasi kwa mawasiliana yafuatayo: 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri na matibabu ya magonjwa mbalimbali sugu.

No comments:

Post a Comment