Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 19 May 2015

LEO NIMEONA NIKUFAHAMISHE HAYA MENGINE ZAIDI KUHUSU NDIZI


Hujambo mpendwa msomaji wetu na wewe mdau wa tovuti hii ya www.dkmandai.com karibu katika muendelezo wa kubadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali ya kiafya pamoja na mimea tiba kwa ujumla.


Leo napenda tujuzane kuhusu ndizi, huenda unafahamu faida za ndizi lakini kama haufahamu basi tumia fursa hii huenda utalipata hata jambo moja ambalo hukuwahi kulijua kuhusu ndizi.

Sote tunaelewa kuwa ndizi mbivu ni tunda maarufu sana lakini pengine ni wachache wanaojua uwezo na faida zake zilizopo kwenye tunda hili.

Kwanza kabisa ifahamike kuwa ndizi ina aina 3 za kipekee za sukari zijulikanazo kama ‘fructose,’ ‘sucrose,’ na ‘glucose’.

Pia ndizi ina kiasi kingi na cha kutosha cha ufumweli yaani ‘fibre’ ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.

Aidha, tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuimarisha nishati ya mwili, hivyo tunda hili linauwezo mzuri wa kuupatia mwili nguvu za kutosha.

Ndizi inavirutubisho vingi ikiwemo protini, ‘potassium’ na vitamin A pamoja na madini ya chuma ambayo husaidia uzalishaji wa hemoglobin katika damu, na hivyo kusaidi kuondoa upungufu wa damu mwilini.

Ikiwa utang'atwa na mdudu, jaribu kusugua sehemu ya ndani ya ganda la ndizi pale ulipong'atwa kwani kwa kufanya hivyo husaidia kupunguza maumivu, uvimbe na kuwasha.

Mbali na kufahamu faida hizo za ndizi inashauriwa kutozihifadhifaida ndizi kwenye jokovu.

Ikiwa ungependa kufika Mandai Herbalist Clinic na kufahamu mengi zaidi kuhusu mimea tiba, mitishamba, nafaka  na matunda ni vyema ufanye mawasiliano nasi kupitia 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment