Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 14 May 2015

LIFAHAMU TUNDA LILILOTANGAZWA KUWA ZAO LA ASILI KWA MWEZI HUU WA MEI.


Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limetangaza tunda la shelisheli kama zao la asili kwa mwezi huu wa Mei.


Tunda hilo la shelisheli limetajwa kuwa na manufaa siyo tu kiafya bali pia na kiuchumi.

FAO inasema kuwa shelisheli ambalo ni zao kuu maeneo ya Pasifiki lina kiwango kikubwa cha wanga na huweza kuliwa bichi au likipikwa.

Kutokana na kiwango kikubwa cha wanga kwenye shelisheli kinalifanya tunda hilo kutumika badala ya unga wa ngano na kutengeneza chapati. Halikadhalika utomvu wake ni tiba ya asili dhidi ya kuhara na magonjwa ya ngozi.

Aidha, mti wa mshelisheli hufaa kwa mbao za ujenzi wa nyumba na mashua na ni thabiti dhidi ya mchwa.

Pia maua ya mshelisheli yanapochomwa moshi wake husaidia sana kufukuza mbu.

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu wa kati mita 9 hadi 18 ambapo huanza kuzaa matunda ukiwa na miaka 6 na kuendelea kwa miaka zaidi ya 50.

Kwa sasa zao hilo ambalo asili yake kabisa ni Ocenia, limeenea hadi maeneo ya Pasifiki, tropikali ikiwemo Afrika, Amerika ya Kusini Australia, Asia na Amerika ya Kusini.


Acha kuteseka na magonjwa anza kupenda afya yako kwa kufika Mandai Herbal Clinic sasa tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam . Tupigie simu namba zifuatazo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment