Monday, 4 May 2015

MAAJABU YA MPERA NA MIZIZI YAKE KATIKA TIBA
Mti wa mpera ni miongoni mwa miti ya matunda ambayo inafahamika vizuri katika jamii ya watu wengi hapa nchini.


Mmea huu kama ilivyo kwa mimea mingine ya matunda, unastawi zaidi katika hali ya hewa ya kitropiki.

Wataalam wa tiba asili wanauzungumzia mti huu kama tiba nzuri inayoweza kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo yale ambayo ni tishio  kwa kizazi cha sasa kama figo.

Mizizi ya mpera ikichemshwa husaidia sana kwa akinamama wenye matatizo ya hedhi au wanaotoa maji maji yenye harufu mbaya kutoka sehemu zao za siri.


Aidha, majani mateke ya mpera yanapofungwa shingoni kwa mwenye tezi yanauwezo wa kuponyesha tatizo hilo pia na mwenye jipu akifunga sehemu husika hulifanya jipu kuiva haraka mno.

Pia kwa wale watoto wadogo wenye matatizo ya kutopata choo zaidi ya siku mbili, wakinyweshwa maji ya majani hayo baada ya kuchemshwa wanapona kabisa tatizo hilo, lakini pia maua ya mpera yanasaidia katika kutibu tatizo la manjano na hata homa kali.

Matumizi ya mizizi na matunda halikadhalika husaidia kuongeza vitamin B na C, ambapo mtumiaji atapaswa kuchemsha majani yenye ujazo wa gramu moja kisha anywe kikombe kimoja mara tatu kwa siku.

Hata hivyo, Dk Mandai anaonya kuwa endapo unasumbuliwa na maradhi hayo ambayo yameelezwa kutibika kwa mti huo wa mpera ni vizuri ukafanya utaratibu wa kuonana naye kwanza kabla ya kuanza tiba hiyo kwa ajili ya maelekezo na ushauri wa kitabibu zaidi. Au piga simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com ili kupata maelekezo zaidi. Au fika kliniki yetu iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment