Wednesday, 6 May 2015

MAAMBUKIZI YA FANGASI KWA WAJAWAZITO
Leo tunaangazia akina mama wajawazito ambao hupata vimelea vya fangasi kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa kinga mwilini.


Hata hivyo, ieleweke kuwa si kila mama mjamzito hupatwa na maambukizi haya ya fangasi aina ya ‘Candida albicans’.

Matumizi ya dawa za kupanga uzazi maarufu kama vidonge vya majira huweza kusababisha mtu kupata maambukizi ya fangasi hawa.

Lakini pia wale wenye upungufu wa kinga mwilini nao huwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa sugu kama saratani, na kisukari.

Wengine wanaopata maradhi haya ni wale waliopata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu mbalimbali au matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo ya uzazi.

Wenye utapiamlo (malnutrition) nao wanaweza kupata tatizo hilo. Wengine wanaoweza kupata ugonjwa huu ni wale wenye tabia ya kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri kama nguo za kuogelea au chupi zilizotengenezwa kwa vitambaa vya nailon au zile zinazobana sana.

Matibabu.
Kabla ya kutibiwa tatizo hili mgonjwa atafanyiwa vipimo vya uchunguzi wa uke ambayo kitaalam huitwa ‘per vaginal examination’ (PV exam) ili kuona kama kuna uvimbe wowote ndani ya utupu huo au kama an maumivu wakati wa kujamiana.

Aidha, daktari pia ataangalia kama kuna uchafu wowote unaotoka na kupima wingi wake, rangi na harufu yake. Uzito wake na aina ya uchafu unaotoka kama ni sahihi kutokana na maelezo ya mgonjwa husika.

Kimsingi daktari atachunguza mambo mengi kama vile kuna uvimbe wowote wa tezi za sehemu ya siri yaani mitoki, shingo ya kizazi, ataangalia sehmu ya haja kubwa ikiwa huenda kuna bawasiri (skin tags)

Hata hivyo mara nyingi huwa inapendekezwa kwamba kabla ya mgonjwa kufanyiwa kipimo ni vyema daktari amjulishe mgonjwa aina ya kipimo, lengo lake na jinsi kitakavyofanyika ili kumuandaa mgonjwa kisaikolojia.

Baadaye daktari anaweza kuchukuwa kipimo na kuotesha kwenye maabara ili kuangalia aina ya uoto huo kama ni fangasi aina ya ‘Candida albicans’ au la.Kama umekuwa ukisumbuliwa na tatizo la fangasi kwa muda mrefu sasa jitahidi ufike Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la tatizo hilo kwa muda mfupi sana. Wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment