Wednesday, 20 May 2015

MADAKTARI WAKICHINA WAPIGWA MARUFUKU KUTOA HUDUMA


Madaktari kutoka nchini China wamepigwa marufuku kuendesha shughuli zao nchini Kongo kutokana na kudaiwa kuwa hawaheshimu sheria za nchi hiyo.

Waziri wa Afya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Felix Kabange amesema kuwa madaktari kutoka China wamepigwa marufuku kuendesha shuhuli zao nchini humo kutokana na madaktari hao kutokuheshimu sheria ya DRC wanapoendesha kazi zao.

Waziri Kabange amesema kuwa serikali imechukuwa uamuzi huo wakupiga marufuku matibabu ya kichina kwa kuwa hospitali zinazoendesha tiba hiyo hazina ruhusa wala mikataba na serikali.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Kabange alisema kuwa wahusika katika tiba za kichina hushirikiana na "wataalamu" wa tiba wanaotia mashaka na kutumia baadhi ya vyakula visivyo ruhusiwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Taarifa ziliendelea kusema kuwa madaktari kutoka China huchanganya tiba ya kisasa, ya kichina na ile ya "jadi" ili kujipatia wateja wengi.Source: TRT- Swahili


No comments:

Post a Comment