Sunday, 17 May 2015

MADAKTARI WALISINZIA WAKIWA KAZINI KILICHOFUATA NI HIKI

Katika mataifa mengi ya Afrika na Marekani Kusini ,kuna uhaba mkubwa wa madaktari jambo linalowalazimu madaktari na wauguzi wachache walioko kufanya kazi ya ziada na kwa muda mrefu ilikuwatunza wagonjwa.


Mara nyingi si ajabu kabisa kumsikia daktari anayehudumu katika hospitali ya umma ndiye yuleyule anayekimbia kumhudumia mgonjwa katika hospital ya kibinafsi iliapate pesa za ziada.

Tumekuwa tukisikia taarifa mbalimbali kuhusu madaktari kufanya makosa ndani ya chumba cha upasuaji na hata mara nyingine katika vyumba vya wagonjwa mahututi kwa sababu ya uchovu.

Daktari akiwa amelala
Huko nchini Mexico wagonjwa na jamaa zao wameanzisha kampeini ya kuwatetea wanafunzi wanaojifunza kazi. Ambao wao waliamua kuwapiga picha madaktari wakisinzia na kuzichapisha katika mitandao ya kijamii.

''inakuaje daktari ambaye anawajibu wa kuwatunza wagonjwa 12 anasinzia kazini ''Hii ni kama rubani kusinzia ndege ikiwa angani '' alisema mwandishi wa blogu aliyechapisha picha hizo.

Daktari akiwa ameuchapa usingizini huku wagonjwa wakimsubiri njeWatu waliochangia mjadala huo katika mitandao ya kijamii walidai kuwa madaktari wakuu wamekwenda kulala na kuwaachia wanafunzi wao kazi nyingi.

Hata hivyo, baada ya mjadala huo katika vyombo vya habari ilibainika kuwa madaktari hao hufanya kazi wakati mwingine hata zaidi ya saa 36 bila mapumziko.

Daktari akiwa amepitiwa na usingizi


Mbali na hayo, wengi waliwashtumu madaktari waliohitimu wakisema kuwa wanawatelekeza wagonjwa wao kufuatia kuimarika maradufu kwa mishahara yao.

Pia  unaweza ukatuambia kama na wewe ulishawahi kushuhudia tukio lolote la daktari kusinzia akiwa katika eneo lake la kazi, tuandikie kupitia ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic-mhc ambapo utaanza kwanza kwa kulike page yetu kisha utaacha ujumbe wako kwenye inbox yetu. Karibu!!

No comments:

Post a Comment