Wednesday, 27 May 2015

MADHARA AMBAYO ANAWEZA KUYAPATA MTOTO ALIYETUMBONI ENDAPO MAMA YAKE ATAKUNYWA POMBE KIPINDI CHA UJAUZITO WAKE


Unywaji wa pombe wa aina yoyote wakati mama akiwa na ujauzito huwa na madhara mbalimbali kwa mtoto aliye tumboni.

Madhara hayo huweza kumkuta mtoto aliye tumboni bila kujali ni kiasi gani cha pombe mama hutumia.

Kumbuka kuwa mama anapokunywa pombe ni sawa na mtoto naye kunywa pia.

Kuna madhara makuu matatu yanayoweza kumsibu mtoto ambaye bado hajazaliwa iwapo mama yake atakuwa anakunywa pombe wakati wa ujauzito.

Kwanza ni uwepo wa hatari kubwa ya kutoka kwa mimba au kuzaliwa mtoto kabla ya miezi tisa.

Pili, chembe za mwili za mtoto aliye tumboni zinaweza kuathiriwa na kusababisha mtoto kuweza kuzali akiwa na ulemavu.

Tatu, chembe za ubongo wa mtoto huyo zinaweza kuharibiwa na pombe na mtoto huweza kuzaliwa akiwa na mtindio wa ubongo.

Ni mara nyingi tumesikia ndugu au hata mume na marafiki wakimshawishi mama mjamzito kwa maneno kama haya " hebu pata kinywaji, kitakuburidisha, kunywa mvinyo kidogo tusherehekee mimba yako. Chupa moja haiwezi kukuathiri bali itakusisimua tu." Kimsingi ushauri huo haufai hata kidogo na huweza kuleta madhara zaidi kwa mtoto aliyetumboni.

Kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu, hebu fanya utaratibu wa kufika ofisini kwetu ili tuweze kutatua tatizo lako la kiafya vizuri kabisa. Pia unaweza kututafuta kwa mawasiliano yafuatayo 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Pia namba hizo za simu zimeunganishwa na whatsapp. Kwa wale wa facebook tupate kupitia ukurasa wetu uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc. 

No comments:

Post a Comment