Monday, 11 May 2015

MAHINDI NAYO NI SEHEMU YA TIBA YA AFYA ZETU


Mahindi ni moja ya zao ambalo hulimwa sana sehemu mbalimbali hapa nchini na zao hili huhesabika kama zao la chakula.


Pamoja na kuwa zao hili kufahamika kama zao la chakula, lakini mizizi yake huweza kuwa tiba kwani husaidia kutibu figo pamoja na kibofu cha mkojo.

Aidha, ndevu za mahindi ni dawa ya maumivu yanayoweza kumpata mtu wakati wa kukojoa pia ndevu hizo husaidia uvimbe wa miguu.

Pia, mmea huo huweza kuwasaidia watu wenye shida katika kukojoa hasa kwa wanaume wazee pamoja na watoto wenye shida ya kukojoa kitandani.

Mizizi hiyo na majani ya mahindi inapowekwa katika maji ya moto na kuchunjwa ndio huweza kuwa tiba.

Mbali na hayo, pia mgonjwa anapochukuwa ndevu za mahindi za kutosha na kuchemsha katika maji kisha kunywa kwa siku tano huwa ni tiba au kinga ya magonjwa tajwa hapo juu.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.   

No comments:

Post a Comment