Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 1 May 2015

MANENO YA BUSARA YA LEO SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI) KUTOKA MANDAI HERBAL CLINIC


Mkurugenzi Mkuu, Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbal Clinic
Ikiwa leo ni May 1, 2015 na ni siku ya maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani, Mandai Herbal Clinic ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dk Abdallah Mandai tunapenda kuungana na wafanyakazi wote hapa nchini na Duniani kwa ujumla kuadhimisha siku hii.


Ambacho tunaweza kusema katika siku hii ya leo ni kuhusu hili la kuzingatiwa masuala yale yote yanayofahamika kuwa ni muhimu katika afya katika mazingira ya kazi hususani maeneo ya viwandani na migodini.

Katika siku hii tunapenda kushauri wahusika (viongozi) wa mashirika, taasisi, makampuni pamoja na viwanda kuhakikisha wafanyakazi wao wanapata hudumu nzuri za kiafya ikiwa ni pamoja na kuwapo kwa huduma ya kwanza katika maeneo ya kazi ili pale inapotokea dharura basi mhusika (mfanyakazi) aweze kupatiwa huduma ya kwanza kabla ya kufikishwa katika kituo cha afya au hospitali. Hili litasaidia sana kupunguza madhara makubwa ikiwemo vifo yasitokee kwa wafanyakazi pindi wanapokuwa katika mazingira yao ya kazi.

Sisi Mandai Herbal Clinic tunajali afya za wafanyakazi na wewe pia anza kujali kwani wafanyakazi wenye afya bora ndio chachu ya mafanikio pia katika, shirika, taasisi, kampuni, kiwanda na nchi nzima kwa ujumla.

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment