Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 20 May 2015

MKOJO NA KINYESI CHA PANYA VIMEELEZWA KUTUMIKA KUTENGENEZEA VIPODOZI
Mara nyingi tumesikia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakipiga vita kuhusu uingizwaji wa bidhaa feki hapa nchini hususani vyakula, dawa na vipodozi ambavyo kwa kiasi kikubwa huathiri afya za watumiaji.


Story kama hizi za bidhaa feki pia zimesikika huko nchini Uingereza ambapo imeelezwa kuwa kinyesi cha panya na mkojo ni baadhi ya viungo vinavyotumika kutengeneza bidhaa feki za urembo kwa wanawake.

Kwa mujibu wa utafiti wa bidhaa za urembo zinazouzwa kwa njia ya mtandao nchini Uingereza umebaini kuwa bidhaa hizo zina tengezwa kwa njia isiyofata maadili na misingi ya kulinda afya za binadamu ikiwemo marashi na mafuta ya kujipaka.

Taarifa ya Polisi waliofanya uchunguzi huo wamebainisha kuwa mfumuko wa bei ya bidhaa kwa njia za kielektroniki umechangia ongezeko la mauzo ya bidhaa hizo.

 ''Ni vigumu sana kubaini uhalali wa bidhaa haswa unaponunua kwa njia ya kielektroniki kwa sababu unachokiona hapo mtandaoni ni picha tu ya bidhaa halali, sasa bidhaa hiyo inapokufikia huwa tayari umekwisha lipia na ni vigumu sana kwako kurejesha bidhaa hizo pindi unapokuwa hujaridhia ubora wake'' alisema afisa aliyesimamia uchunguzi huo.

Polisi pia wanasema kuwa uchunguzi wao umegundua kuwa marashi ghushi yanayouzwa London yanajumuisha sumu aina ya 'cyanide' na mkojo wa binadamu.


Mbali na hayo, imeelezwa kuwa bidhaa za kielektroniki zinazopendelewa na wafanyabiashara walaghai ni kama zile ambazo hutumika kusokota nywele na zile ambazo zinazotumika kwa ususi.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa bidhaa hizo huwa haziwezi kuhimili matumizi ya muda mrefu na hivyo zinahatarisha maisha ya watumiaji kutokana na hatari ya kulipuka.

Source:BBC
Asante kwa kuendelea kuwa karibu nasi na kufanya tovuti yetu kuwa moja ya sehemu yako ya kupata habari. Pia unakaribishwa kutangaza nasi biashara yako yoyote. Tupigie simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com gharama zetu ni nafuu sana

No comments:

Post a Comment