Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 6 May 2015

MMEA WA MLIWA UNAPOTUMIKA KATIKA KUTUNZA NGOZI YAKOMmea wa liwa unaaminika kuwa asili yake ni nchini India na huko ndiko unapendwa na kutumika sana.


Kwa hapa nyumbani Tanzania mti huu tunauita ‘Mliwa’ ambapo leo tunauangazia faida zake mbalimbali katika tiba.

Unga wa liwa unapochanganywa na maziwa husaidia kutibu ugonjwa wa kisonono na matatizo ya sehemu za mkojo na sehemu za siri.

Aidha, liwa pia imekuwa ikitumiwa na wanawake wa Tanzania visiwani katika kuwapamba maharusi wanapoolewa.

Kimsingi matumizi ya liwa hayana historia ya kusababisha madhara yoyote kwa mtumiaji zaidi ya kuwa na faida kama kuondoa vipele, chunusi na kumfanya mhusika kuwa mng’avu bila kudhuru ngozi.

Hata hivyo, baada ya kupaka liwa unashauriwa kutopaka kitu kingine usoni ikiwemo poda, krimu kwa kuwa ukipata vitu hivyo wakati wa usiku vitundu vya ngozi huziba na kushindwa kuingiza hewa vizuri mwilini na hivyo kusababisha ngozi kusinyaa na kukosa hewa.

Liwa inaweza kupakwa mwili mzima, lakini hasa usoni ambapo kunaonekana kwa haraka ili uweze kuifanyia yako iwe na mvuto na kupendeza.

Liwa haichubui uso wala kukufanya uwe mweupe bali liwwa inakufanya kuwa na ngozi yenye kung’ara zaidi na kukuweka katika hali ya kupendeza wakati wote.

Hata hivyo, wataalam wa masuala ya urembo wanashauri kuacha ngozi ipumzike wakati wa usiku bila kuweka kitu chochote chenye kemikali kwa ajili ya kufanya ngozi yako iwe nyororo na ya kupendeza maana mchana mara nyingi ngozi husinyaa kutokana na joto la mwili.

Liwa hupakwa bila kujali kuwa mhusika ni mweusi au mweupe kifupi haichagui kwa kuwa ni kwa ajili ya kung’arisha tu na wala si ya kujichubua, liwa inaweza kupakwa kutwa ara mbili au hata zaidi kwa kuwa haina madhara yoyote katika ngozi ya binadamu zaidi ya kuiweka ngozi kuwa katika hali nzuri zaidi.

Sambamba na hayo, ukihitaji kumuandaa bibi harusi, liwa inaweza kutumika kwa kupakwa wiki nzima kabla kwa ajili ya kumwandaa kwa sherehe ya kwenda kuolewa.

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.  

No comments:

Post a Comment