Sunday, 24 May 2015

MTI WA MUAROBAINI NA UWEZO WAKE KATIKA KUTIBU MAGONJWA YA NGOZI


Muarobaini ni mti ambao unauwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali na umekuwa ukiaminika hivyo kwa miaka kadhaa hivi sasa.

Leo tutaangalia namna juisi ya muarobaini inavyoweza kusaidia katika kutibu magonjwa mbalimbali.

Muarobaini una uwezo mkubwa wa kuzuia na kutibu ‘allergy’ (mzio) za aina tofauti kwa kupaka juisi yake mwilini pamoja na kunywa.

Aidha, mti huu unaelezwa kuwa na uwezo wa kupambana na saratani pamoja na kuimarisha kinga ya mwili. Hii ni kutokana na tindikali ziitwazo ‘Polysaccharides’ na ‘limonoids’ ambazo huatikana katika magamba, majani na mizizi, hivyo husaidia sana katika kuboresha kinga ya mwili, na kuufanya mwili kuwa na kinga imara zaidi.

Mti huu pia umekuwa na sifa ya kusaidia kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi yakiwemo mapunye, upele, pamoja na mba nk.

Hali kadhalika muarobaini pia husaidia damu kutembea vizuri kwenye mishipa vile inavyotakiwa na hivyo kusaidia mapigo ya moyo kwenda vizuri zaidi.

Pamoja na hayo, muarobaini pia unauwezo wa kuua fangasi, ikiwa unatatizo la fangasi miguuni, kwenye maungio ya siri, unaweza tumia juisi ya muarobaini kwa kujipaka sehemu zilizoathirika hii itakusaidia kupambana na fangasi hao bila madhara.


Mbali na hayo, muarobaini pia ni dawa ya kufukuza wadudu wakiwemo mbu.

Kabla ya kutumia mmea huu ni vyema kuwasiliana na mtaalam wa tiba silia au mtu mwenye uelewa mzuri kuhusu tiba asilia ili kupata maelekezo zaidi.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment