Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 7 May 2015

MVUA YAVUNJA DARAJA DOGO LA MBAO, KISHA KILICHOTOKEA NI VIJANA KUANZA KUPOPOANA MAWE NA MBAO, NIMEKUWEKEA STORY YOTE NA PICHA ZA TUKIO


Kweli walimwengu hawana shukrani, hii imetokea baada ya daraja dogo linalounganisha kati ya eneo la Ukonga, Mombasa na Mongolandege kuvunjika kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, ambapo baadhi ya vijana wenye nia mbaya wameonekana wakitumia maafa hayo kuiba mbao za daraja hilo badala ya kuokoa mbao hizo zisiondoke na maji.
Kamera yetu ya www.dkmandai.com ilifika eneo la tukio mapema asubuhi ili kujionea hali ya daraja hilo na kukuta baadhi ya vijana waliokuwa upande wa ukonga Mombasa wakiwa katika daraja hilo huku wakitoa mbao moja baada ya nyingine na wengine wakisikika wakisema kuwa boda boda lazima mlale na njaa mwaka huu kutokana na daraja hilo kuwa kivuko kikubwa cha madereva bodaboda wanapowapeleka wateja wao.

Katika hali ya kushangaza zaidi vijana hao walipoona wameanza kumulikwa na kamera yetu walianza kurusha mawe na mbao kwa lengo la kuzuia kamera yetu isiwachukue.

Baada ya vijana hao kuanza kurusha mawe hayo kukazuka majibizano ya kutupiana mawe na mbao kati ya vijana wa upande wa Ukonga, Mombasa na vijana wa Mongolandege ambapo hadi nusu saa inapita wakati tukiondoka eneo la tukio bado makundi hayo ya vijana walikuwa wakiendelea kurushiana mawe na mbao hizo.

Baada ya muda viongozi wa mtaa na wazee wenye busara walifika na kuanza kuwatuliza vijana hao, lakini hali bado ilionekana kuwa tete , kwani vijana walizidi kurushiana mawe zaidi, na hivyo kupelekea wazee hao kuwasiliana na Jeshi la Polisi ili kupata usaidizi zaidi.

Hata hivyo, hadi wakati tunaondoka eneo la tukio polisi walikuwa bado hawajawasilia na vijana hao walikuwa wakiendelea kushambuliana.

Itakumbukwa kwamba daraja hilo dogo ambalo ni kiunganishi kikubwa kati ya wakazi wa eneo la Ukonga, Mombasa na Mongolandege lilijengwa kwa msaada mkubwa wa Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic baada ya daraja kubwa la serikali kuharibika siku za nyuma.

Picha zaidi za tukio hilo zipo hapa chini.Vijana wakiwa katika harakati za kuiba mbao za daraja hilo
Sambamba na hayo Mamlaka ya hali ya hewa imesema kuwa mvua hizo bado zitaendelea leo na kesho, hivyo tahadhari zaidi imetakiwa kuendelea kuwepo miongoni mwa watanzania wa maeneo mbalimbali  hapa nchini.

Endelea kuwa karibu na tovuti hii kwa habari mbalimbali zikiwemo na za kijamii pia.

No comments:

Post a Comment