Monday, 11 May 2015

EWE MZAZI TUMIA NJIA HIZI KUONGEZA KIASI CHA UTOKAJI WA MAZIWAKuna baadhi ya wanawake wanapojifungu hujikuta wakiwa na tatizo la kutoa maziwa hafifu yaani ambayo hayatoshelezi mahitaji ya mtoto.

Hivyo kutokana na kuthamini kwetu maisha ya watoto na afya za watoto kwa ujumla leo Mandai Herbal Clinic tunakufahamisha hizi njia mbili ambazo huweza kumsaidia mama kuongeza kiasi cha maziwa.

Kwanza kabisa mzazi mwenye tatizo hili anaweza kutumia kitunguu swaumu kama suluhisho la tatizo hilo. Jambo la kufanya ni kuhakikisha unatengeneza supu ya vitunguu swaumu punje mbili au tatu, kisha ongeza vijiko vitatu vya mezani vya asali.

Baada ya kukamilika mchanganyiko huo mama atapaswa kunywa kila asubuhi kwa ajili ya kuongeza utoaji wa maziwa.

Kama njia hiyo ni ngumu, pia unaweza kutumia ufuta kijiko kimoja cha chai cha ufuta. Weka ndani ya lita moja ya maji. Chemsha kwa muda, baada ya muda kupoa (vuguvugu) chuja na apewe mzazi anywe yote.

Pia ni vyema kula ufuta kwa ajili ya kuongeza utoaji wa maziwa.
  
Asante kwa kuendelea kuwa karibu nasi, lakini kama unatatizo lolote la kiafya unaweza kuonana na Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbal Clinic, Dk, Abdallah Mandai kila siku ya Jumatatu hadi Jumapili ofisi, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au piga simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment