Saturday, 23 May 2015

MZAZI AMPELEKA MTOTO WAKE WA SIKU MBILI KWA MGANGA WA KIENYEJI KILICHOTOKEA NI UNYANYASAJI WA HALI YA JUU (VIDEO)


Matukio ya ukatili dhidi ya watoto wadogo yamekuwa yakiendelea ulimwenguni, ambapo leo katika harakati zangu za kupitia taarifa mbalimbali duniani kupitia mitandao nimekutana na hii stori ya mtoto wa siku mbili kunyanyaswa huko nchini India ikanilazimu kushare na wewe mdau wetu.

Unyanyasaji wa mtoto huyo umetokea baada ya mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Rakesh Kumar, ambaye ni mganga wa kienyeji huko nchini India kuamua kumlazimisha mtoto wa siku mbili kutembea akiamini kuwa atapona.

Inaelezwa kuwa mtoto huyo alikuwa akisumbuliwa na homa kali na wazazi wake waliamua kumpeleka kwa mganga huyo ambaye alimchukua mtoto na kumlazimisha kutembea akiwa uchi huku akiwa amemkaba koo.

Hata hivyo, licha ya tukio hilo kutendeka mbele ya umati wa watu, lakini hakuna hata mmoja aliyeamua kutoa msaada kwa mtoto huyo ambaye alikuwa akilia sana baada ya kitendo hicho cha kulazimishwa kutembea.

Kutokana na tukio hilo mama mzazi pamoja na mganga huyo walifunguliwa mashitaka na mtoto huyo alipelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.Chanzo: Millardayo.com

No comments:

Post a Comment