Tuesday, 26 May 2015

MZAZI TUMIA NJIA HIZI KUMSAIDIA MTOTO WAKO KUONDOKANA NA TATIZO LA KUKOSA CHOO (CONSTIPATION)
Watoto wadogo hususani wale ambao bado wananyonya na wale ambao ndio wameanza kula vyakula vingine zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na tatizo hili la kuwa na choo kigumu na hata kukosa choo kabisa.

Kukosa choo au kupata choo kigumu ni hali ambayo kitaalam huitwa ‘constipation’ hali hii huweza kuwakuta watu wazima na hata watoto pia, lakini leo tutaangali kwa watoto.
Mara nyingi tatizo hili huwakumba watoto wale ambao tayri wanakuwa wameanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama.

Wataalam wanashauri tatizo hili linapomkuta mtoto wako ni vyema kwanza kumuona daktari pindi unapogundua mtoto wako anasumbuliwa na tatizo hili.

Pia unaweza kujaribu kutumia njia hizi zifuatazo ili kuondokana na tatizo hilo;

Mpatie mtoto maji safi na salama ya kutosha na utakuwa ukipunguza kiwango au kuongeza kiasi cha maji kulingana na hali ya mtoto inavyokuwa ikiendelea.

Pia unaweza kumpatia mtoto juisi za matunda pamoja na kumpa vyakula vyenye nyuzi nyuzi endapo mtoto atakuwa ameshaanza kula vyakula vigumu.

Mbali na hayo, unaweza kumpaka mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Hakikisha mafuta unayotumia si yale yenye madini (mineral oil.)

Kwa ushauri na matibabu zaidi ya magonjwa mbalimbali, tafadhali fika ofisini kwetu Mandai Herbalist Clinic iliyopo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo: 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. No comments:

Post a Comment