Saturday, 9 May 2015

NDIMU NA UWEZO WAKE KATIKA KUONDOA MBA


Kwa kawaida weekend huwa ni wakati mzuri ambao wengi huutumia kwaajili ya kupumzika nyumbani baada ya shughuli nyingi za wiki nzima.

Hivyo na mimi leo nakusogezea hivi vitu muhimu kwa ajili ya weekend, moja ya mambo muhimu katika weekend ni kuonekana nadhifu zaidi na hauwezi kuwa nadhifu endapo nywele zako zinashida ya mba.

Leo kuna hii mbinu ya kuzuia mba katika nywele zako wewe mwanamama, kitu cha kufanya ni rahisi sana ni wewe kuwa na ndimu tu.

Jinsi ya kuandaa chukuwa ndimu yako ikamue kisha upate kijiko kimoja cha mezani cha maji ya ndimu kisha changanya kwenye glasi moja ya maji ya kawaida.

Baada ya kuosha nywele zako vizuri suuza nywele zako kwa kutumia maji yenye mchanganyiko wa ndimu, hii ni tiba kwa ajili ya magonjwa ya ngozi kichwani na kufanya nywele zikue kwa haraka.


Asante sana kwa kuendelea kuwa karibu nasi, kama unatatizo lolote la kiafya unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na pia unahaki ya kuwasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Kisha utatuambia tatizo lako nasi tutakuwa tayari kuweza kukusaidia.

No comments:

Post a Comment