Saturday, 30 May 2015

NJIA HII ASILI ITAKUSAIDIA KUTIBU KIKOHOZI


Huenda wiki hii nzima umekuwa ukisumbuliwa na tatizo la kikohozi, hivyo weekend hii nimeona ni vyema nikupe hii mbinu ya asili itakayokusaidia kuondokana na tatizo hilo

Unachopaswa kufanya ni kumenya punje 4 za kitunguu swaumu, kisha utavikata katika mtindo wa vipande vidogo vidogo.

Baada ya kufanya hivyo utachanganya vipande hivyo vya kitunguu swaumu na kikombe kimoja cha asali na uuache mchanganyiko huu ukae usiku mzima.

Asubuhi utachukua kijiko kidogo kimoja cha mchanganyiko huu na ulambe mara 2 kwa siku hadi pale utakapo pona.

Kwa ushauri na matibabu zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa mawasiliana yafuatayo: 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment