Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 11 May 2015

ONDOSHA UCHOVU KWA KUFANYA MAMBO HAYA


Kuchoka huweza kuchangiwa na sababu nyingi, inaweza kuwa ni kwasababu ya kufanya kazi nyingi au nzito bila kupumzika au kufikiri sana kwa muda mrefu bila kutuliza akili.
Kuchoka ni dalili ya kuonesha na kudhihirisha kuwa mwili wako unahitaji mapumziko.


Zipo hapa njia mbalimbali za kukusaidia kuondoa uchovu unapokuwa umechoka.

Jipumzishe kwa kulala mahali safi na tulivu
Kiafya unatakiwa kulala kwa muda wa saa 6-8 na si vinginevyo. Kwa wakati wa mchana, unaweza ukajipumzisha kwa kusinzia kwa dakika chache 10-15.

Kumbuka lengo la kulala ni kuupumzisha mwili na ubongo ili upate nguvu na kuongeza ufanisi wake wa kiutendaji kazi.

Kunywa kinywaji laini au kula chakula chepesi chenye kukupa nguvu.
Maji au juisi fresh ya matunda ni nzuri sana, unapokunywa kinywaji laini mwili wako unapata nafasi ya kurudisha na kufidia maji yaliyopotea mwilini na hatimaye kurejea katika hali nzuri.

Sikiliza muziki utakaokufanya ujiliwaze.
Muziki unaweza kukuondolea msongo wa mawazo na kujihisi vizuri mwenye furaha. Kusikiliza wimbo na kucheza peke yako ni njia moja wapo ya kujichangamsha hasa pale unapofuatilia maneno yanayoimbwa katika wimbo huo

Uzuri wa muziki ni pale unapoimba na kwenda sambamba na ujumbe wa kile kinachoimbwa. Fanya hivyo na baada ya burudani utajikuta hali yako imebadilika na kuwa nzuri kabisa.

Fanya mazoezi madogo
Kutokana na uchovu kusababisha jointi na viungo vingine kama kiuno kukaza. Ondoa tatizo hilo kwa kufanya zoezi la kujinyoosha.

Tulia mahali penye hewa safi upunge upepo.
Njia nyingine ni kukaa au kutulia mahali penye upepo mwanana kwa dakika kadhaa. Kaa sehemu yenye uwazi mkubwa wa kusimama na kuangalia mandhari mazuri ya mahali ulipo.

Cheza michezo ya kukuburudisha
Kwenye simu za mkononi au computer kuna michezo kwaajili ya kujiburudisha.

Tumia angalau dakika kadhaa kucheza game kwenye computer au simu yako ili kuiburudisha akili kisha uendelee na mambo yako mengine.


Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.    

No comments:

Post a Comment