Wednesday, 27 May 2015

PAMOJA NA KUWA NA UMRI MKUBWA WA MIAKA 65, LAKINI ALIFANIKIWA KUPATA WATOTO PACHA WA 4


Si kawaida kusikia mwanamke mwenye umri wa miaka zaidi ya 60 kuendelea kupata watoto hususani katika mika hii ya sasa ambapo swala la uzazi limekuwa ni tatizo kidogo kwa kinamama wengi.

Lakini leo kuna hii stori nyingine kutoka nchini Ujerumani ambapo bibi wa miaka 65, Annegret Raunigk amefanikiwa kujifungua watoto wanne mapacha, watatu wakiwa wakiume na mmoja wa kike.

Daktari aliyemzalisha mama huyo kwa njia ya upasuaji alisema watoto hao walizaliwa wakiwa hawajatimiza miezi sita baada ya kufikisha wiki 26 lakini walizaliwa wakiwa na hali nzuri kiafya ya kuendelea kuishi.

Mama huyo tayari ana watoto 13 na wajukuu saba na ameingia kwenye rekodi baada ya kuwa mwanamke mzee aliyefanikiwa kubeba mimba ya watoto pacha wanne katika umri wake huo.

.

No comments:

Post a Comment