Tuesday, 26 May 2015

PAPA FRANCIS AMESEMA HAJAWAHI KUTAZAMA TV KWA MIAKA 25 SASA


Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutazama runinga kwa miaka 25 sasa.

Papa Francis alisema mara ya mwisho alitazama runinga tarehe 15 mwezi Julai mwaka wa 1990.

Najua utajiuliza ni kwanini kiongozi huyo wa kidini duniani ameamua kuishi hivyo,lakini yeye anasema alifikia uamuzi huo wa kutotazama runinga baada ya kumuahidi Maria Mtakatifu kuwa angekoma kushiriki uraibu huo.

Mbali na kutoangalia runinga, pia Papa Francis amesema huwa hatumii mtandao wa intaneti na badala yake yeye anasema kuwa huwa anatenga dakika 10 tu kwaajili ya kusoma gazeti la kiitaliano.

Papa Francis vilevile hufuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu wake ambao humsimulia yanayojiri.

Swali linakuja kwako wewe mdau wetu, Je unaweza kukaa mbali na Runinga yako, Simu yako ama mtandao wa Intanet kwa siku ngapi ?

 Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment