Tuesday, 5 May 2015

PARACHICHI HUUKINGA MWILI DHIDI YA SUMU

Parachichi ni tunda linalosika kwa kuwa na virutubisho vingi na linaloupatia mwili vitamini C. 


Tunda hili hupatikana kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Mbeya.

Aidha, tunda hili pia limekuwa likitumiwa na wanawake  mbalimbali katika kudumisha masuala ya urembo kwa kupaka usoni, au nywele.

Parachichi lina faida nyingi kiafya, hususani kuukinga mwili dhidi ya kemikali hatari pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana.

Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Michoacana de San Nicolas de Hidalgo cha nchini Mexico wanaeleza kwamba tunda hilo husaidia katika kuukinga mwili dhidi ya kemikali hatari (free radicals), hivyo kuweka kinga dhidi ya magonjwa mengi pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana.

Wanasayansi hao wanaeleza kuwa mafuta yanayopatikana katika parachichi yana uwezo wa kupenya hadi ndani ya injini inayotengeneza nishati mwilini inayopatikana katika seli inayojulikana kama mitochondria.

Kwa mujibu wa wataalamu hao, free radicals ni kemikali zinazosababisha magonjwa mengi yakiwamo baadhi ya saratani, kuharibu mishipa ya damu ya ateri arteries, pamoja na kumfanya mtu kuzeeka haraka.

Kwa muda mrefu wanasayansi wamekuwa wakiita parachichi kama mfalme wa matunda kutokana na kuwa na virutubisho vingi kuliko tunda jingine lolote duniani.

Kutokana na umuhimu wa parachichi, kuna haja ya kujenga utamaduni wa kuala tunda hili endapo linapatikana kirahisi kwa manufaa ya afya zetu.

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment