Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 4 May 2015

PINDA AHIMIZA ELIMU YA ATHARI ZA MADAWA YA KULEVYA


Waziri Mkuu Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, amewataka viongozi wa dini zote nchini katika nchi kutumie mikutano yao ya mahubiri kutoa elimu juu ya athari za madawa ya kulevya kwa waumini wao na Watanzania wote kwa ujumla.
Aidha, Pinda amewataka viongozi wa dini nchini kuungana na serikali kwa ajili ya kutoa elimu juu ya athari za biashara ya madawa ya kulevya na matumizi yake katika jamii, huku akiongeza  kuwa, kampeni hiyo inapaswa kuanzia misikitini, makanisani na kwenye mikutano yote inayofanywa na viongozi wa dini na wa serikali.
Mbali na hayo, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa, viongozi wa dini wana jukumu kubwa la kuwalea zaidi vijana ili wasijiingize kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu wao ndiyo kundi kubwa zaidi miongoni mwa waumini.

No comments:

Post a Comment