Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 15 May 2015

SI KAWAIDA KUTOKEA NA INAPOTOKEA LAZIMA ITAKUSHANGAZA, NI HII STORY YA DAKTARI KUSAHAU SIMU KWENYE TUMBO LA MAMA MJAMZITO


Moja ya habari kubwa iliyosikika kwenyevyombo vya habari mbalimbali Ijumaa ya leo Mei, 15, 2015 ni hii story ya daktari kusahau simu ndani ya tumbo la mama mjamzito.

Mara kadhaa tumekuwa tukisikia stori kutoka vyombo mbalimbali vya habari duniani vikiripoti kuhusu stori za madaktari kusahau mkasi au baadhi ya vifaa tiba ndani ya tumbo la mama lakini hii ya kusahau simu huenda ikawa ni yakushangaza zaidi.

Kwa mujibu wa Gulf News tukio hilo limetokea nchini Jordani ambapo inaelezwa kuwa mama huyo aliyekumbwa na tukio hilo anatambulika kwa jina la Hanan Mahmood na aligundua hali hiyo baadaya simu kuanza kuunguruma tumboni mwake.

Taarifa zinasema kuwa daktari huyo ambaye pia alikuwa kiongozi wa upasuaji alisahau simu yake ya mkononi kwenye tumbo la mama huyo mjamzito, alipokuwa akimfanyia upasuaji mama huyo ambaye alienda kujifungua.

Hata hivyo, Hamna Mahmood ambaye alikuwa na umri wa miaka 36 alijifungua mtoto wa kiume akiwa na uzito wa Kg 4.8
Karibu uanze kutangaza nasi sasa kupitia tovuti hii yenye kutembelewa na watu wengi zaidi. Tupigie simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Gharama zetu ni nafuu sana.

No comments:

Post a Comment