Friday, 22 May 2015

SI KILA UNACHOPELEKA MDOMONI NI KIZURI KWA AFYA YAKO, VINGINE HUWA NA MADHARA YA TARATIBU

Magonjwa mbalimbali na hasa yale yasiyoambukizwa mara nyingi husababishwa na namna tunavyoishi hususani katika masuala ya mlo.

Siku za hivi karibuni magonjwa kama saratani mbalimbali, matatizo ya moyo, kisukari yamekuwa yakumba watu wengi zaidi na hii ni kutokana na sababu ya vyakula vinavyosababisha magonjwa mbalimbali, na mbaya zaidi vyakula hivyo ndivyo huliwa zaidi kuliko vingine.


Leo kupitia Mandai Herbalist Clinic tumeona ni vizuri tukuletee orodha ya baadhi ya vyakula ambavyo vinaaminika kusababisha magonjwa hatari hususani saratani.

Utumiaji wa vyakula vya kukaanga
Mara nyingi vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya, ikiwa ni pamoja na mhusika kuwa na uwezekano wa kuweza kupata saratani ya kwenye mfuko wa uzazi. Mfano wa vyakula hivyo ni pamoja na chips na vingine ambavyo hupikwa kwa kukaangwa kwenye mafuta.


Matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi
Vyakula vyenye chumvi nyingi navyo huweza kusababisha saratani, kwani inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa saratani tumboni. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni kama vile vya kusindika, mfano nyama za makopo, maharage, n.k


Kutumia sukari kupita kiasi.
Matumizi mabaya ya sukari yamekuwa yakielezwa kusababisha saratani. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa katika vinywaji mbalimbali, mfano juisi soda, mara nyingi vinywaji hivyo huwa nasukari nyingi inayoweza kupelekea saratani ya kongosho. Sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula

Unywaji wa pombe
Unywaji wa pombe kupita kiasi nao unaelezwa kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake na waume. Aina ya saratani zinazowezwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya ini, utumbo na koromeo.

Matumizi ya nyama na mafuta
Watu wanaopenda kula nyama kila siku, huweza kuwa katika hatari ya kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja na kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, uligundua kuwa watu wanaopenda kula nyama kila siku wako katika hatari ya kupatwa na saratani hiyo.


Hivyo ni baadhi ya vyakula vinavyoweza kukusababishia maradhi mbalimbali na hasa ya saratani, hivyo ni vizuri kuzingatia ulaji wa vyakula vya asili vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku.
Ikiwa ungependa kufika Mandai Herbalist Clinic na kufahamu mengi zaidi kuhusu mimea tiba, mitishamba, nafaka  na matunda ni vyema ufanye mawasiliano nasi kupitia 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment