Saturday, 2 May 2015

SIFA ZA CHUNGWA NI KUWA NA VITAMINI C, JE, UNAIFAHAMU HII SIFA NYINGINE YA TUNDA HILO KATIKA TIBA? NIMEKUWEKEA HAPA KARIBU!Mara nyingi tumeshasikia sana kuhusiana na chungwa kuwa na sifa ya kuwa na vitamin C nyingi na kuwasikia wataalam wakishauri ulaji wa tunda hilo.


Lakini leo Jumamosi nimeona nikuletee hizi faida za kemikali iitwayo 'limonoids' ambayo pia inapatikana katika chungwa.

Kemikali hii ya limonoids inaelezwa kuwa na uwezo wa kuusaidia mwili katika kupambana na aina mbalimbali za saratani kama vile saratani ya matiti, tumbo na utumbo mkubwa, ngozi.


Aidha, ni vyema ikafahamika kuwa chungwa moja kubwa au mawili madogo yanatosha kumpa mtu mahitaji yake ya vitamini C kwa siku na endaoutakosa chungwa basi unaweza kutumia vyakula vingine kama mboga za kijani, pilipili nyekundu, nyanya, broccoli na spinachi ambazo nazo zinauwezo wa kuupa mwili vitamin C.

Pamoja na hayo ifahamike kuwa kwa kawaida mwili hauna uwezi wa kutengeneza vitamini C wala kuuhifadhi, hivyo kwa mantiki hiyo ni vizuri kila siku ukapata mlo wenye vitamini C. 

Mbali na hayo, juisi ya machungwa nayo inasaidia kuzuia magonjwa ya figo na vijiwe katika figo. Hata hivyo, unywaji wa juisi usipite kiasi hata kama ni juisi ya asili kama machungwa. Unywaji mwingi wa juisi za matunda asili au za kiwandani unaweza kuongeza wingi wa sukari katika damu, na hivyo kuongeza unene kupita kiasi na kuchosha homoni ya insulini, inayodhibiti maradhi ya kisukari.

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 


No comments:

Post a Comment