Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 19 May 2015

TABIBU MANDAI LEO ANAKUFAHAMISHA DALILI AMBAZO HUASHIRIA MWANAMKE KUWA NI MJAMZITO


Baadhi ya wanawake na mabinti wengi wamekuwa wakiwasilina nasi kupitia ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic –mhc pamoja na barua pepe yetu ya dkmandaitz@gmail.com na jambo kubwa wamekuwa wakiomba kufahamu dalili zinazoashiria kuwa ni wajawazito.


Hivyo leo nimeona ni vyema niandae orodha ya dalili hizi kisha niwapatie kwa faida ya wale waliouliza lakini pamoja na wadau wetu wote kwa ujumla.

Kwanza kabisa ifahamike kuwa dalili hizi za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine.

Kimsingi dalili moja kubwa kabisa ya kuwa mwanamke huenda tayari kashika ujauzito ni hii ya mwanamke kukosa hedhi yake au kuchelewa kupata hedhi.

Dalili na viashiri vingine ni pamoja na mwanamke kuhisi uchovu. Wengi hujikuta wakihisi hali hii na kujikuta ni wazito wa kufanya shughuli mbalimbali za kila siku.

Kuvimba matiti au kuhisi maumivu, hii huweza kutokea kati ya wiki ya kwanza hadi ya pili.Pia wengine hutokewa na hali ya kubadilika rangi katika ngozi inayozingira chuchu na kuwa na rangi nyeusi.

Kupata kichefuchefu na kutapika, huku wengine hujikuta wakipata maumivu ya kichwa na kupatwa na kizunguzungu.

Kupata haja ndogo mara kwa mara hususani katika kipindi cha wiki 6 hadi 8 .

Kuanza kuchagua vyakula na kushindwa kula baadhi ya vyakula ambapo awali alikuwa akivitumia bila shida.

Kuwa na tabia ya kuchukia mara kwa mara na kwa haraka hata kama si jambo la kusababisha kuchukia.

Pamoja na dalili hizo zote inapofika wiki ya ishirini mama huweza kupata alama kama ya mstari mweusi ambao hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu.

Pia mama huweza kuanza kuhisi maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.

Hizo ndio baadhi ya dalili ambazo huweza kumpata mwanamke mwenye ujauzito, hivyo endapokama unahisi ni mjamzito ni vyema ukawahi katika kituo cha afya kilicho karibu na mahali unapoishi kwa uchunguzi zaidi na kufahamu hali halisi ya ujauzito wako.

Ikiwa ungependa kufika Mandai Herbalist Clinic na kufahamu mengi zaidi kuhusu mimea tiba, mitishamba, nafaka  na matunda ni vyema ufanye mawasiliano nasi kupitia 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment