Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 18 May 2015

TAFITI: MAZOEZI YANA NAFASI KUBWA YA KUONGEZA MIAKA MITANO ZAIDI YA KUISHI


Mara kadhaa tumekuwa tukiambiana kuhusu umuhimu wa kuzingatia kufanya mazoezi na kutenga angalau dakika 30 za mazoezi kila siku.


Sasa kuna hii taarifa ya utafiti uliofanyika hivi karibuni ni vyema ikufikie kwani imebainika kwamba watu wanaofanya mazoezi ya kila mara wana nafasi kubwa ya kuishi kwa miaka mitano zaidi ya wale ambao hawafanyi mazoezi yoyote.

Utafiti huo uliowajumuisha watu waliokomaa pia umebaini kuwa watu walio na umri mkubwa wanauwezo wa kuishi maisha marefu zaidi pindi wanapoacha kuvuta sigara.

Utafiti huo wa miaka 11 uliwajumuisha watu wazima 5,700 nchini Norway na ulidhibitisha kuwa watu waliofanya mazoezi kwa takribani saa tatu kwa juma wanaishi zaidi ya miaka mitano zaidi ya wale ambao hawakufanya mazoezi yoyote.

Kutokana na utafiti huo imewalazimu wanasayansi hao kuanzisha kampeini za kuhamasisha faida za kufanya mazoezi hasa kwa watu wazima.

Pamoja na hayo, wanasayansi hao waliandika katika jarida moja la utabibu wa michezo linalochapishwa nchini Uingereza, huku wakisema kuwa maisha ya kuketi bila ya kuwa na shughuli yoyote inayochemsha damu mwilini huchangia kwa kiwango kikubwa kuzorota kwa uwezo wa mwili kuhimili dhoruba ya maambukizo tofauti tofauti haswa mtu anapozeeka.

Pia Chuo kikuu cha Oslo nacho kilithibitisha kufuatia utafiti huo kuwa hata mtu akifanya mazoezi mepesi ni kheri kuliko kukosa mazoezi kabisa.

Takwimu za utafiti zinaonesha kuwa watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wakishiriki mazoezi yoyote kwa dakika 150, hiyo hutosha kabisa kumweka mtu katika hali nzuri ya kiafya.

Aidha kwa wale wenye umri kati ya miaka 68 hadi 77 wanahitaji kufanya mazoezi kwa zaidi ya saa moja kwa juma ilikupata manufaa yake.

Kwa ujumla asilimia 40% ya washirika waliofanya mazoezi kwa takriban nusu saa kila siku walikuwa bado hai katika utafiti huo uliodumu kwa miaka 11.

Mbali na hayo, ripoti hiyo iliongezea kusema kuwa hata wale wazee waliokuwa na miaka 73 walipoanza mazoezi asilimia kubwa walikuwa hai zaidi ya wenzao ambao hawakufanya mazoezi yeyote.

Source: BBC
  
Acha kuteseka na magonjwa anza kupenda afya yako kwa kufika Mandai Herbal Clinic sasa tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam . Tupigie simu namba zifuatazo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment