Wednesday, 20 May 2015

UWEZO WA KARAFUU KATIKA KUTOA AHUENI KWA WENYE PUMU


Pumu ni tatizo la kupumua ambalo mara nyingi huwapata watoto na hata watu wazima kutokana na hitilafu mbalimbali katika mfumo wa kupumua.


Pumu huweza kusababishwa na kuvimba kwa kingo za mirija ya kuvuta hewa, matatizo ya mzio (allergy), matatizo ya uyeyushaji wa chakula ndani ya tumbo pamoja na matatizo ya kisaikolojia.

Tatizo hili la pumu likishughulikiwa vizuri kwa watoto wadogo huweza kuisha kabisa.

Tiba ya pumu hailengi katika kuponya kabisa, ila husaidai kufifisha nguvu ya mashambulio ya pumu pale yanapotokea, pia kumbukuza kwa kiasi kikubwa idadi ya mashambulio ya pumu kwa mgonjwa.

Moja ya njia inayoweza kutoa ahueni kwa mgonjwa wa pumu ni pamoja nah ii ya kutumia karafuu na asali.

Chukua punje 6 za karafuu na zichemshe kwa muda wa dakika 5 hadi 7. Ongeza asali vijiko viwili vya mezani kisha koroga vizuri.

Baada ya kufanya hivyo gawanya dawa hiyo katika sehemu tatu zinazolingana na kisha kunywa dawa hiyo asubuhi mchana na jioni.

Kumbuka: Tiba ya pumu ni ya kuendelea

Pamoja ya ushauri na matibabu hayo pia ni vyema mgonjwa kujitahidi kuepuka kila jambo ambalo linaonekana kuchochea ugonjwa wa pumu. Pia ni vyema kuwasiliana na mtaalam wa tiba asilia kabla ya kuanza tiba hii ili kupata ushauri zaidi.

Ikiwa ungependa kufika Mandai Herbalist Clinic na kufahamu mengi zaidi kuhusu mimea tiba, mitishamba, nafaka  na matunda ni vyema ufanye mawasiliano nasi kupitia 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Namba zetu hizo pia zinapatikana kwenye whatsapp. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam 

No comments:

Post a Comment