Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 19 May 2015

WAGONJWA WAKATISHWA UHAI WAO NA MUUGUZIUnapokuwa unaumwa na kuamua kwenda hospitali mara nyingi huwa tunaamini hiyo ni sehemu sahihi kabisa ya usalama wa maisha yako kutokana na imanizetu kwa wauguzi pamoja na madaktari, lakini hali inapokuwa tofauti ni kufanya sehemu hizi za hospitali nazo kutokuaminika hali inaweza kuwa mbaya zaidi.Nimeanza kwa kusema hivyo kutokana na hii story kutoka nchini Uingereza ya muuguzi mmoja kuhukumiwa kwa makosa ya kuwaua wagonjwa wake wawili na kuwapa wengine 20 sumu katika hospitali ya Greater Manchester.

Muuguzi huyo aliyefahamika kwa jina la Victorino Chua alimuua Tracy Arden, mwenye umri wa miaka 44, na Derek Weaver mwenye umri wa miaka 83 katika hospitali ya Stepping Hill kwa kuwatilia sumu wagonjwa katika dawa zao.

Inaelezwa kuwa dawa zilizotiwa sumu baadaye zilitumiwa na wauguzi wengine ambao hawakujua mshtakiwa alikuwa amezichafua.

Hata hivyo, Chua aliondolewa kosa jingine la tatu la mauaji, lakini akahukumiwa kwa makosa mengine mengi dhidi ya wagonjwa wake ikiwa ni pamoja na lile la mgonjwa mmoja kujeruhiwa ubongo wake.

Aidha, muuguzi huyo Chua hakupatikana na kosa la kumuua Arnold Lancaster, mwenye umri wa miaka 81, lakini akapatikana na hatia ya kumwekea sumu kwenye dawa.

Hata hivyo, Chua hakuonesha hisia zozote wakati wa hukumu yake ilipokuwa ikitolewa na atatangaziwa kifungo chake Jumanne ya leo.

Inaelezwa kuwa wagonjwa hao waliwekewa sumu kati ya Juni, 2011 na Januari, 2012.

No comments:

Post a Comment