Thursday, 28 May 2015

WAKATI WENGINE WANALIA KWA KUKOSA WATOTO MAMA HUYU YEYE HIKI NDICHO ALICHOFANYA KWA MTOTO WAKEKuna baaadhi ya matukio ukiyasikia ni lazima utajiuliza mara mbili au mara tatu ikiwa ni kweli yametendwa na baadhi ya wanawake, ambao mara zote wamekuwa ndio nguzo ya upendo wa watoto katika jamii.

Miongoni mwa matukio hayo ni haya ya unyanyasaji dhidi ya watoto wadogo ambao wengi wetu huwafananaisha na malaika.

Leo kuna hii stori nyingine kutoka huko Ufilipono, ambapo kuna mama kaamua kumfunga mtoto wake mnyoyoro shingoni kisha kumuwekea chakula kama mbwa kwa madai kuwa mtoto huyo amekua akimsumbua.
Mama huyo aliweka picha za mwanaye huyo wa kiume akiwa uchi kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, na baadaye picha hizo zilichukuliwa na wanaharakati wa haki za binadamu na kumfungulia mashtaka.


Hata hivyo, mmoja wa wanaharakati hao Lurleen Hilliard. alisema kwa sasa mtoto huyo atakua chini ya kituo cha kulelea watoto wakati mama yake akitumia adhabu kwa unyanyasaji alioufanya.


Tuwapende watoto, kumbuka kuwa wewe unayemnyanyasa mtoto wako leo kuna mwenzio ana mwaka wa tatu au watano sasa analia kwa Mwenyezi Mungu kwa kukosa mtoto na hajui ni lini atafanikiwa kumpata.

No comments:

Post a Comment