Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 18 May 2015

WANAWAKE AMBAO SI BIKRA HAWANA HAKI YA KUPATA KAZI YA JESHI INDONESIA


Kumekuwa na utaratibu unaowalazimisha wanawake nchini Indonesia kuthibitishwa endapo kama bado ni bikra au la kabla ya kujiunga na jeshi la taifa hilo.


Kutokana na utaratibu huo nchini wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameibuka na kuhimiza Serikali ya Indonesia kukomesha kipengele hicho cha kubainisha iwapo mwanamke ni bikira au la kabla ya kujiunga na jeshi la taifa hilo.

Wanaharakati hao wanasema kuwa kitendo hicho huwadhalilisha wanawake hao kwa misingi ya kijinsia.

Aidha, shirika la Human Rights Watch (HRW) limeongeze, kwamba mtu kuwa au kutokuwa bikira hakuathiri utendaji kazi na uwajibikaji wa mwanamke kazini.

Wanaharakati hao pia wamesema kuwa wengi wa makurutu ambao huwa ni wasichana waliohitimu shule ya upili wenye umri kati ya miaka 18-20 hulazimika kukaguliwa sehemu zao za uzazi ilikuthibitisha endapo wangali  ''wasafi na hivyo wazalendo''

Wengi wangeoenda kufahamu kipimo hicho ni namna gani hufanyika, taarifa ni kwamba “kulingana na mtafiti mmoja Andreas Harsono kipimo hicho kijulikanacho kama "two-finger test", kinatumika na madaktari ili kubaini iwapo mwanamke ni bikira au la”

Kinachofanyika ni ''daktari anatumbukiza vidole viwili ndani ya uke na kimoja katika tupu ya nyuma ''alisema mama mmoja mke wa mwanajeshi ambaye pia ni askari.
Hata hivyo, hadi sasa haijabainika faida ya kipimo hicho ambacho kinalaumiwa kuwa kinawadhalilisha wanawake. Huku Amiri Mkuu wa Jeshi la Indonesia Meja Jenerali Fuad Basya, yeye akisema kuwa kipimo hicho ni nguzo ya uzalendo na swala muhimu katika usalama wa taifa.

''Haiwezekani iwapo mtu ni msherati si muaminifu kwa mumewe apewe jukumu la kulinda usalama wa taifa'' alisema Meja Jenerali Fuad.

Aliongeza kwa kusema kuwa “kama mtu anapania kulinda mipaka ya taifa na pia usalama wa mamilioni ya watu ilihali ameshasaliti nafsi ya mumewe basi mtu kama huyo hapaswi kupewa jukumu la kulinda taifa''
Mbali na hayo, Meja Jenerali Fuad alinukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza kuwa ''kama mwanamke si bikira iwe amegonjeka ama amejamiani hafai kuwa askari hafai kuhudumu katika jeshi la Indonesia ''

Hata hivyo, majibu ya Jenerali yalitofautiana na ya mke mmoja wa mwanajeshi ambaye mwenyewe ni askari aliyesema kuwa walipewa sababu tofauti ya kipimo hicho.ikiwamo hii ''Wajua jeshi la Indonesia linataka wanajeshi wenye siha nzuri kwa hivyo wanalazimika kutumia mbinu kama hizo kupunguza gharama za matibabu ''

Pamoja na hayo, Shirika la afya Duniani WHO limepinga sheria hiyo likisema haina misingi yoyote ya kiafya.

Source: BBC

No comments:

Post a Comment