Wednesday, 27 May 2015

WATU 13 WAFARIKI KUFUATIA MVUA KUBWA NCHINI MEXICO


Mafuriko yanapotokea katika nchi yoyote ni sawa na janga tu, kwani mara kadhaa tumeshashuhudia mafuriko hapa nchini ambayo yamekuwa yakisababisha uharibifu mkubwa wa makazi ya watu, miondombinu, upotevu wa mali pamoja na vifo pia

Leo kuna hii story kutoka huko Ciudad Acuna mpakani mwa Marekani na Mexico, ambapo mvua kubwa imenyesha na kupelekea watu 13 kufariki na wengine kuyahama makazi yao.

Kufuatia mvua hiyo maelfu ya nyumba zimebomoka na zaidi ya watu 1,900 wameokolewa na kupewa hifadhi katika jimbo la Texas nchini Marekani.

Naye, Waziri wa Mambo ya Ndani, Victor Zamora, katika jimbo la Coahuila alisema kuwa watoto watatu walifariki katika mafuriko hayo, huku watu wengine watano hawajulikani walipo.

No comments:

Post a Comment