Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Saturday, 16 May 2015

WAZAZI WAHOFIA MABINTI ZAO KUPATA MIMBA WAKIWA SHULENI WALICHOAMUA SASA NI KUWADUNGA SINDANO ZA KUZUIA MIMBA TU!!


Wanawake nchini Kenya wameonekana kutokuwa tayari kupata wajukuu mapema na kuamua kuwadunga sindano za uzazi wa mpango watotot wao wa kike.

Hofu hiyo imeonekana zaidi kwa kinamama waishio ambao hivi sasa wanawapa watoto wao wa kike wenye miaka 12 sindano za uzazi wa mpango wakihofu kuwa mabiti zao watapata ujauzito na kukatiza masomo.

Mmoja wa Ofisa wa Wizara ya Afya, Wycliffe Onkendi alieleza kuwa “wazazi hao hivi sasa wanajaribu kila njia za uzazi wa mpango ili angalau mabinti wamalize elimu ya sekondari’’

Kwa mujibu wa gazeti la The Standard matumizi ya njia za uzazi wa mpango kunamaanisha kuwa wanawake hawa wamekubali kuwa mabinti zao wajihusisha na ngono zisizo salama wangali na umri mdogo. Hofu yao hasa imejikita katika madhara ya kupata mimba zisizopangwa kabla ya kumaliza masomo.

Mary Agak, ambaye ni mama na mfanyabiashara mjini Kericho anasema “ binti yangu yuko kidato cha tatu huwa tunaongelea maswala haya mara chache na wanawake wengine kwenye chama sioni kama ni makosa. Kabla ya kuingia kidato cha tatu nilimpeleka kuchomwa sindano ambayo ilikaa kwa miezi mitatu mpaka minne ni vijana wadogo damu inachemka huwezi jua watafanya nini’’.

Naye mama mwenye watoto watatu anaongeza kuwa ‘’bora nizuie balaa hili kuliko kumshuhudia asimalize shule’’.
Ofisa mmoja katika zahanati moja mjini, Eldoret Paul Anyango anasema ‘’mabinti walio sekondari hufika kwenye kituo hicho cha afya wenyewe kwa ajili ya kupata vipandikizi au sindano wanapokwenda shuleni’’

Hali hii inafanya watu kujiuliza mabinti hawa hufanya nini zaidi ya masomo wanapokuwa shuleni.

Karibu uanze kutangaza nasi sasa kupitia tovuti hii yenye kutembelewa na watu wengi zaidi. Tupigie simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Gharama zetu ni nafuu sana.

No comments:

Post a Comment