Saturday, 23 May 2015

WAZEE WA KINYEREZI WAMEAMUA KUMUALIKA DK MANDAI KWENYE UZINDUZI HUU WA KLABU YAO (PICHA)

Wazee wanaoishi katika wilaya ya ilala eneo la Kinyerezi- Zimbili Jumamosi hii wamefanya uzinduzi wa klabu ya wazee na kumualika Dk Mandai katika uzinduzi huo.

Klabu hiyo ambayo imezinduliwa rasmi leo na Dk, Abdallah Mandai, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala kiitwacho Mandai Herbalist Clinic kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na kupatiwa jina la 'TUPO SAWA KLABU YA WAZEE' ni klabu ambayo itawaruhusu wazee mbalimbali kujiunga bila kujali itikadi za kisiasa wala kidini.

Akizungumza katika uzinduzi huo Dk. Mandai ametoa pongezi nyingi kwa wazee hao kwa kuamua kuanzisha umoja huo na kusema kuwa ni nadra sana kuona wazee wakianzisha kitu chao wenyewe kutokana na wazee wengi kuwa na mtazamo kuwa mtu anapozeeka kinachofuata ni kifo tu.

Pia Dk Mandai amewataka wazee hao kutokata tamaa juu ya kile walichoanzisha, huku akisema kuwa "kwa sasa mtatumia nguvu nyingi katika kuimarisha umoja huu, lakini siku zote dhamira ya kweli ndio itakayokupeleka mbele na siku zote uwazavyo ndivyo hivyo huwa kama unawaza kuwa masikini basi usitarajie kuwa tajiri na kama unawaza kuwa mgonjwa basi usidhani utakuwa mwenye afya"

Katika uzinduzi wa klabu hiyo, Dk, Mandai ameamua kuchangia kiasi cha shilingi milioni tatu, ikiwa kama moja ya njia ya kuisaida klabu hiyo kuanza vyema.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mohamed Mashine, amesema kuwa wamefikia uamuzi wa kufungua klabu hiyo ya wazee wakiwa na malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaidiana juu ya masuala mbalimbali yakiwemo ya kijasiriamali pamoja na kubadilisha mawazo pia

Aidha, akifafanua zaidi kuhusu namna ya kujiunga katika klabu hiyo Mwenyekiti Mashine alisema hapo awali kabla ya uzinduzi huo kufanyika leo kujiunga ilikuwa ni bure kabisa, lakini kwa sasa kila mwanachama atakayehitaji kujiunga itabidi atoe kiasi cha shilingi elfu kumi na tano ili kuingia katika klabu hiyo.

Pamoja na hayo, mwenyekiti ametoa shukrani za dhati kwa Dk Mandai na baadhi ya wageni wengine waliohudhuria katika uzinduzi huo.

 Picha za matukio zaidi katika uzinduzi huo
Dk Mandia akisaini kwenye kitabu maalum cha wageni
Dk Mandai akifungua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi klabu hiyo
Msomaji  lisala (kushoto) akiwasilisha mbele ya mgeni rasmi
Dk Mandai akisikiliza kwa makini lisala
Dk Mandai akipokea pongezi mara baada ya kuhitimisha kuongea
Dk Mandai alipofika alipokelewa na wazee vyema kabisa
Baadhi ya wazee na wanachama waliokuwa sehemu ya uzinduzi huo

Kinamama nao hawakuwa nyuma
Mandai Herbalist Clinic tunapenda kuwatakia kila jema umoja wa wazee wa  'TUPO SAWA KLABU YA WAZEE, na waweze kusonga mbele na kudumisha umoja huo.

No comments:

Post a Comment