Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 8 May 2015

ZAMBARAU NAUWEZO WAKE DHIDI YA UGONJWA WA KISUKARI


Habari za leo msomaji wetu wa www.dkmandai.com napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha katika muendelezo wetu wa kufahamishana namna mimea na matunda yanavyoweza kuwa msaada mzuri katika afya zetu.
Leo napenda kuzungumzia namna zambarau inavyoweza kuwa msaada kwa mtu mwenye ugonjwa wa sukari.

Lakini kwanza ni vyema ifahamike kuwa kisukari ni ugonjwa unaotokana na matatizo ya mfumo wa uyeyushwaji wa chakula ndani ya mwili. Ukosefu au upungufu wa kemikali inayoitwa insulin husababisha ongezeko la kisukari inayojionesha kwa kiwango kikubwa katika mkojo wa mwathirika.

Pia ni vyema ikafahamika kuwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari hayalengi katika kuuponyesha ugonjwa, ila kumsaidia mgonjwa aweze kuishi maisha ya kwaida.

Matumizi ya zambarau huweza kumpa ahueni mgonjwa wa kisukari, ambapo kinachopaswa kufanyika ni kukausha mbegu za zambarau, kisha saga ili kupata unga laini.

Baada ya kufanya hivyo tumia nusu kijiko cha chai cha unga huo wa zambarau katika nusu glasi ya maji kila siku asubuhi kabla ya kula chakula chochote.

Asante sana kwa kuendelea kuwa karibu nasi, kama unatatizo lolote la kiafya unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na pia unahaki ya kuwasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Kisha utatuambia tatizo lako nasi tutakuwa tayari kuweza kukusaidia.

No comments:

Post a Comment