Monday, 4 May 2015

ZIFAHAMU HIZI FAIDA 6 UTAKAZOPATA PALE UTAKAPOTUMIA MBEGU ZA MABOGAMaboga hutokana na tunda liitwalo boga, tunda ambalo asili yake haifahamiki vizuri ni wapi, ingawaje baadhi ya tafiti zinasema kuwa asili yake ni Amerika ya kaskazini.Zao la maboga mara nyingi hushamiri zaidi katika msimu wa joto na inashauriwa kupanda zao hili mwanzoni mwa mwezi Julai hasa katika udongo unaotunza maji vizuri.

Leo ninayo furaha kukufahamisha hizi faida sita za kutumia mbegu za maboga.

Saratani ya kibofu
Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha zinki, tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.

Kinga ya mwili
Mbegu za maboga zina kiwango cha madini aina ya zink, ambayo pia yana faida nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na na uimarishaji wa kinga mwilini , ukuaji wa seli, macho na ngozi ya mwili. Hali kadhalika zinki huimarisha nguvu za kiume.


Huimarisha moyo na mifupa
Mbegu za maboga huwa kiwango kingi cha madini aina ya magnesium, ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na uimarishaji wa mifupa pamoja na mishipa ya damu sambamba  na kuongeza ufanisi wa utumbo mpana . Magnesium inaonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshtuko wa moyo na kiharusi.

Uvimbe
Mbegu za maboga zimeonesha kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, ikiwa ni pamoja na kuvimba miguu, vidole na hata majipu.


 Ugonjwa wa ini
Mbegu za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na hayo mbegu hizi zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.


Usingizi
Kwa watu wenye matatizo ya kukosa usingizi, wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja na tunda lolote muda mfupi  kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha kwamba mbegu za maboga zina kirutubisho kinachohamasisha uzalishaji wa homoni za usingizi kwa wingi
 

Mbegu hizi huweza kufanya vizuri endapo zikitumika zikiwa hazijaoza na zilizo safi na ambazo hazijakaa muda mrefu, lakini pia tumia mbegu hizo kwa usalama zaidi ikiwa ni sambamba na kuziosha na maji safi na salama kisha zianike na inapendeza zaidi ukila bila kukaanga, lakini ukila pia baada ya kukaanga bado utapata faida zake. Isipokuwa hakikisha haziungui wakati unapozikaanga unaweza kutumia dakika 10 tu katika zoezi hilo la kuzikaanga.


Kama ungependa kuyafahamu mambo mengi zaidi kuhusu tiba asilia kwa kutumia mimea, matunda nafaka na mitishamba endelea kuwa karibu na tovuti hii au like ukurasa wetu wa facebook unaofahamika kama Mandai Herbal Clinic- mhc kisha utakuwa ukifikiwa na taarifa zetu mbalimbali kila siku. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo; 0717 961 795/ 0653 163 838 / 0754 391 743. Barua pepe dkmandaitz@gmail.com
No comments:

Post a Comment