Thursday, 21 May 2015

ZIPO HAPA FAIDA ZA KUTUMIA MIZIZI YA MLONGE


Mlonge ni mti wenye historia ndefu sana hasa katika masuala ya tiba. Karibu mti wote huu wa mlonge ni dawa.


Leo nataka kukwambia hizi faida za kutumia mizizi yake ambazo huweza kukusaidia katika kutibu maradhi mbalimbali.

Mizizi ya mti mchanga wa mlonge ni tiba nzuri ya mishipa ya fahamu , kifafa pamoja na tatizo la baridi yabisi sugu.

Mizizi ya mlonge iliyopondwa na kisha kuwekwa chumvi na kubandikwa kwenye uvimbe wowote wa viungo husaidia sana pamoja na wale waliopooza.

Mtu mwenye maradhi ya koo, pia anaweza kuchemsha mizizi ya mlonge na kutumia maji yake kusukutua.

Ikiwa ungependa kufika Mandai Herbalist Clinic na kufahamu mengi zaidi kuhusu mimea tiba, mitishamba, nafaka  na matunda ni vyema ufanye mawasiliano nasi kupitia 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Namba zetu hizo pia zinapatikana kwenye whatsapp. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam   

No comments:

Post a Comment