Friday, 1 May 2015

ZIPO HAPA SABABU ZA KUKUFANYA KULA SAMAKISamaki ni miongoni mwa kitoweo ambacho hupendwa na watu wengi na kutumiwa na watu mbalimbali hususani wale wa kanda ya ziwa.

Aidha, licha ya kitoweo hiki kupendwa na watu wengi pia ni moja ya kitoweo chenye virutubisho vingi mwilini.

Miongoni mwa virutubisho hivyo vinavyopatikana katika samaki ni pamoja na aina ya Omega 3 ambavyo husaidia katika kuulinda moyo dhidi ya maradhi.

Aidha, samaki pia wanasifika kwa kuwa na virutubisho ambavyo humuongezea mlaji uwezo wa kukumbuka vizuri pamoja na virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na saratani mwilini.

Pia ulaji wa samaki husaidia kuongeza kinga mwilini na kuondoa mafuta mabaya mwilini, hivyo unashauriwa kula samaki kwa wingi kadiri uwezavyo.

Mbali na faida hizo za ulaji wa samaki pia unapotumia samaki husaidia kumpatia mlaji protini, vitamini B3, vitamin D, vitamini B6,  Omega 3 Fatty Acids. 


Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.
 

No comments:

Post a Comment