Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 30 June 2015

AJALI YA NDEGE YA KIJESHI YAUA WATU 100 INDONESIAUokozi ukiendelea mara baada ya ajali hiyo
Kuna ajali nyingine huwa hazitokei mara kwa mara, lakini pale zinapotokea huwa na madhara makubwa zaidi.

Leo kumekuwa na taarifa ya takriban watu 100 kufariki dunia baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.

Kufuatia ajali hiyo maafisa wa kijeshi wanasema kuwa tayari miili 49 imepatikana katika eneo la ajali.

Wakielezea kuhusu ajali hiyo maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wamesema kwamba, ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.

Ndege hiyo ilipoanguka ilikuwa imebeba mizigo aina ya Hercules 130 na ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 113 ilipoanguka.

Hata hivyo, taarifa mbaya zaidi kutoka kwa Afisa Mkuu wa Jeshi la Wanahewa Air Marshall Agus Supriatna, amesema kuwa hakuna manusura waliopatikana hai.

Ndege hiyo iliangukia majengo kadhaa na kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.

Msemaji wa jeshi la angani alisema kuwa rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.

Shukrani kwa kuendela kuungana nasi mdau wetu, pia tunapenda kukukaribisha kutangaza biashara yako kupitia website hii, gharama zetu ni nafuu sana. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment