Thursday, 25 June 2015

ALIPUKIWA NA SIMU AKIWA ANAZUNGUMZA NDANI YA GARI, NJIA YA HARAKA YA KUJIOKOA IKAMBIDI AIRUSHE NJE!!!


Hivi inakuaje pale ambapo unatumia simu, halafu katikati ya maongezi yakakatizwa kutokana na simu yako kulipukia?

Sasa huko nchini India mtu mmoja aitwaye Kishan Yadav , ameripotiwa kulipukiwa na simu yake ya iPhone 6 wakati alipokuwa akizungumza nayo.

Yadav alilipukiwa na simu hiyo ya iPhone 6 iliyotoa cheche za moto, baada ya kuzungumza nayo kwa muda mrefu.
Tukio hilo lilitokea wakati Yadav alipokuwa akizungumza na simu hiyo, huku akiwa ndani ya gari na ilipoanza kuteketea Yaday alirusha simu yake nje .

Kufutatia tukio hilo kampuni ya Apple imeichukuwa simu hiyo ya iPhone 6 kwa ajili ya ukaguzi, na kuamrisha maafisa wa usalama kuanzisha uchunguzi.

 Unaweza kuwasiliana nasi kwa maelezo zaidi au ushauri, piga simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment