Tuesday, 2 June 2015

ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA BADO INAHITAJIKA KWA UMMA


Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Mara kwa mara tumekuwa tukizungumzia juu ya namna mimea inavyoweza kuwa tiba ya magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu.

Hivyo endapo siku moja mimea yote itatoweka kwa kukatwa hivyo huenda tukapoteza baadhi ya mimea tiba mingi nchini na kuishia kuendelea kuathiriwa na magonjwa huku tukikosa tiba.

Kutokana na kulitambua hilo Makamu wa Rais wa Tanzania, Mohammad Gharib Bilal, amesema kuna haja ya elimu ya umma kutolewa mara kwa mara kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ili Watanzania wafahamu umuhimu wa jambo hilo.

Makamu wa rais ameyasema hayo jana kwenye hotuba yake kwa katika siku ya mazingira duniani, ambapo amesema kuwa, Tanzania inakabiliwa na hatari ya kupoteza baadhi ya mimea na wanyama kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na watu wanaofuatilia maslahi yao binafsi.

Aidha, makamu wa rais ameongeza kuwa, ukataji wa miti ni moja ya matatizo aliyosema yanaipeleka pabaya Tanzania na kusisitiza kuwa hali hiyo isipodhibitiwa, matokeo yake yake yataviathiri vizazi vya sasa na vijavyo.

Kila mwaka, Juni mosi imetengwa kuwa siku ya mazingira duniani na serikali za dunia hutumia siku hiyo kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.

Mbali na hayo pia Umoja wa Mataifa umesema uharibifu wa mazingira ndio uliopelekea kutokea kwa mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yameleta matokeo mabaya kama vile ukame katika baadhi ya nchi na mafuriko pia.

No comments:

Post a Comment