Friday, 19 June 2015

FAHAMU KUHUSU UMUHIMU WA MAFUTA YA NAZI


Mafuta ya nazi husaidia sana kwa kutibu magonjwa mbalimbali hasa magonjwa ya ngozi.

Leo nimeona ni vizuri tufahamisane baadhi ya matatizo ambayo huweza kumalizika kwa kutumia mafuta ya nazi.

Mafuta ya nazi husaidia sana kwa wale wenye matatizo ya fangasi, kinachohitajika ni kupata mafuta ya nazi na maji ya mchai chai, kisha tumia maji mchanganyiko huo mara mbili kwa siku kwa kupaka sehemu iliyoathirika. Fanya hivyo hadi pale tatizo lako litakapoisha.

Mafuta ya nazi pia husaidia kuondosha madoa na muwasho kwenye ngozi, hivyo kukuacha katika muonekano mzuri zaidi. Paka mafuta ya nazi mahali ngozi ilipoathirika mara mbili kwa siku hadi pale utakapoona mabadiliko.

Pia mafuta haya husaidia sana pale unapooumwa na wadudu kama vile nyuki, au siafu. Paka mafuta ya nazi kwenye eneo ulilong’atwa. Fanya hivyo mara mbili kwa siku hadi utakapo pona.

Matumizi ya mafuta ya nazi husaidia kuondoa harufu mbaya ya mwili ni pale yanapotumika kujipaka. Inashauriwa kutumia mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni na baada ya wiki kadhaa utaona mabadiliko.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu ni vyema ukafanya uamuzi sahihi wa kufika Mandai Herbalist Clinic ili kuonana na Tabibu Abdallah Mandai na kuweza kupata matibabu sahihi. Unaweza kupiga simu namba; 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika moja kwa moja ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.  

No comments:

Post a Comment