Friday, 19 June 2015

FAHAMU NAMNA YA KUTIBU KIKOHOZI KWA KUTUMIA BIZARI


Kikohozi ni moja ya ugonjwa unaowasumbua wengi hasa katika mwezi huu wa Juni, tatizo hili limekuwa likichangiwa sana na mabadiliko ya hewa au majira tuliyonayo kwa sasa.

Lengo la kukohoa ni kutoa chembechembe zisizohitajika katika njia ya kupitisha hewa na kwa kawaida kikohozi cha kawaida huweza kupona hata bila dawa ya aina yoyote.

Zifuatazo ni badhi ya tiba za kikohozi.

Bizari
Pata kijiko kimoja cha unga wa bizari kisha weka ndani ya sukari na kanga kidogo, baada ya hapo ongeza maziwa nusu glasi, kisha endelea kupasha moto kwa muda wa dakika tatu.

Baada ya hapo epua mchanganyiko huo, kisha weka ndani ya kikombe na uongeze asali kijiko kimoja cha chai kisha kunywa.

Tiba hii ifanyike mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu.

Asali.

Tumia asali kijiko cha mezani mara tatu kwa siku, asubuhi, mchana na usiku kwa muda wa siku tatu hadi saba

 Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu ni vyema ukafanya uamuzi sahihi wa kufika Mandai Herbalist Clinic ili kuonana na Tabibu Abdallah Mandai na kuweza kupata matibabu sahihi. Unaweza kupiga simu namba; 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika moja kwa moja ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.  

No comments:

Post a Comment