Tuesday, 2 June 2015

FENESI LINAPOTUMIKA NA KUWA TIBA


Fenesi ni miongoni mwa matunda yenye ladha tamu, lakini pia tunda hili linatajwa kuwa na faida nyingi endapo litatumika vizuri.

Tunda hili linatajwa kuwa ni chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu.

Fenesi pia ni chanzo kizuri cha vitamini C. Hivyo kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo tunda hilo husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua na mafua.

Pamoja na hayo pia tunda hili husaidia kurekebisha msukumo wa damu na kurahisisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa mawasiliana yafuatayo: 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri na matibabu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu. 

No comments:

Post a Comment