Saturday, 20 June 2015

HII NAYO KALI MASHINE ZA BVR ZASAFIRISHWA KWA BODABODA MWANZA!!


Ofisa uandikishaji ambaye hakufahamika jina lake akitumia pikipiki kusafirisha mashine ya BVR jana katika barabara ya ya Mwanza - Shinyanga.( Picha na Goodluck Ngowi)
Na Goodluck Ngowi
Mwanza

IMEELEZWA kuwa bajeti ndogo iliyopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maafisa wake wa uandikishaji inasababisha kusafirisha mashine hizo kwa kutumia pikipiki kitu ambacho kinachangia uharibifu wa mashine za BVR kwa baadhi ya vituo.

Kauli hiyo imekuja baada ya kituo cha uandikishaji cha Mahina Kanyerere kusitisha uandikishaji kwa muda baada mashine waliyokuwa wakiitumia kuharibika tangu juzi.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu jana, (kwa sharti la kutotaja jina lake) Afisa uandikishaji wa kituo kimoja jijini hapa alisema kuwa usafiri wanaotumia kwa kusafirisha mashine hizo sio salama kutokana na miundombinu ya baadhi ya maeneo.

"Kiwango cha bajeti tulichotengewa ni kidogo hivyo tunasafirisha mashine hizi kwa kutumia bodaboda na barabara zenyewe ndio hizi mbovu kwa nini mashine zisiharibike?" Alihoji Afisa huyo.

Ofisa uandikishaji ambaye hakufahamika jina lake akitumia pikipiki kusafirisha mashine ya BVR jana katika barabara ya ya Mwanza - Shinyanga.( Picha na Goodluck Ngowi)
 Naye mkazi wa eneo hilo, Jeremiah Zadock, alisema kuwa mashine katika kituo chake iliharibika hivyo toka jana wameshindwa kujiandikisha.

"Watu tunashindwa kufanya shughuli nyingine za maendeleo kutokana na ubovu wa hii mashine toka jana (juzi) na hatuna uhakika hiyo nyingine italetwa lini maana siku zenyewe zimebaki nne," alisema Zadock.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo, Willium Kasingongo, alithibitisha kuwepo kwa tatizo hilo na kudai kuwa ameshawasiliana na viongozi wa ngazi za juu ili kupata uwezekano wa mashine nyingine na kuwataka wananchi wa hapo kuwa wavumilivu.
  
Shukrani kwa kuendelea kupitia tovuti hii mara kwa mara, tambua tunathamini sana uwepo wako msomaji wetu, tunaomba uendelee kuwa nasi kila siku kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali 

No comments:

Post a Comment