Friday, 19 June 2015

HIVI UNAJUA NI WATU WANGAPI WAMESHAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA MACHAFUKO NCHINI BURUNDI?


Ikiwa ni mwezi moja na nusu sasa tangu kuanza kwa maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza.

Shirika la haki za binadamu na za wafungwa Aprodh, limetangaza Alhamisi Juni 18 kwamba machafuko hayo yanayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi yamesababisha vifo vya watu 70 mpaka sasa.

Hii ni ripoti ya kwanza ambayo inaonesha idadi hiyo kubwa ya watu waliouawa katika maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Kiongozi wa shirika hilo, Pierre-Claver Mbonimpa, ameeleza idadi hiyo ya watu 70 waliyouawa ambayo ni kubwa kuliko ile inayojulikana mpaka sasa ya watu 50.

“ Mpaka sasa tunahesabu idadi ya watu 70 ambao wameuawa. Kuna watu wengine 500 ambao walijeruhiwa, na tuna idadi ya watu zaidi ya 500 wanaozuliwa katika jela tofauti. Kuna baadhi ya watu ambao wanazuliwa katika jela za polisi na Idara ya upelelezi ”, amesema Pierre-Claver Mbonimpa.

Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka tovuti hii ya www.dkmandai.com, lakini inapofika wakati utajisikia haupo vizuri kutokana na kuumwa basi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.  

No comments:

Post a Comment